BOT: Marufuku Kukopesha Bila Leseni

BOT: Marufuku Kukopesha Bila Leseni

General / 25th November, 2022

Benki Kuu ya Tanzania imebaini kuwa kuna baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila leseni, Jambo ambalo ni kinyume na kifungu  cha 16(1), cha sheria ya huduma ndogo ya fedha yam waka 2008.


Hivyo Benki Kuu inapendaa kuutaarifu umma kuwa, taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha.


Aidha kwa mujibu wa mujibu wa kifungu cha 16(2)(a) cha sheria ya huduma ndogo ya fedha  mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa sheria hiyo, ni pamoja na faini ya shilingi Milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka miwili.


Hata hivyo Banki Kuu ya Tanzania imewaasa wananchi kuepuka kufanya biashara na kukopa kwa taasisi, watu binafsi ambao hawana leseni.


Na orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biasshara ya kukopesha zilizotolewa na banki kuu ya Tanzania  inapatikana kwenye tovuti ya banki kuu ambayo ni www.bot.go.tz.