BoT kuchukua hatua kudhibiti mfumuko wa bei nchini

BoT kuchukua hatua kudhibiti mfumuko wa bei nchini

General / 23rd November, 2022

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florence Luoga amesema kuwa kuimarika kwa Sekta ya Benki nchini kunatokana na usimamizi mzuri wa Benki Kuu ambayo ndio muangalizi Mkuu wa Sekta hiyo, ambayo imekuwa ikichangia kuifanya iweze kuchagiza katika ukuaji wa uchumi. 

Prof. Luoga ameyasema hayo Novemba 22,2022 katika Chuo cha Benki Kuu Jijini Mwanza wakati wa mahojiano na waandishi wa habari katika Mkutano wa siku mbili wa mawasilisho ya mada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maafali ya kwanza ya Chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25, mwaka huu.

Amesema hatua hiyo imetokana na uwepo wa waatalamu wa uendeeshaji katika Sekta hiyo ambao wamechangiza kueendelea kuimarika kwa sekta ya benki ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Prof. Luoga amesema kuwa Benki hiyo imeendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha mfumuko wa bei haukui na kuleta athari za kiuchumi kwa Taifa.

Amesema kuwa mfumuko wa bei Tanzania bado ni mdogo ambao ni asilimia 4.8 ikilinganishwa na nchi nyingine za Bara la Afrika na Ulaya ambazo hivi sasa zinakaribia asilimia 10 na zaidi na kwamba Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti mfumuko wa bei kutokana na wataamu wake kufanyakazi kwa weledi kuhakikisha kunakuwepo na udhibiti wa viashiria vitakavyosababisha kuwepo kwa athari hiyo.

“Kwa Tanzania kuwa na mfumuko wa asilimia 4.8 hiyo sio bahati bali imetokana na wataalamu wetu wanavyoweza kuangalia viashiria vya mfumuko wa bei kuongezeka ghafla na kuchukua hatua ya kuhakikisha mfumuko wa bei hautokei kwa ghafla hiyo.  Kwa hiyo kuna hatua maalum ambazo sisi tunazichukuwa Ili kuilinda nchi dhidi ya mfumuko wa bei” amesema Profesa Luoga.


Gavana wa Benki Kuu ya tanzania (BoT) Prof. Florence Luoga akizungumza alipokuwa katika Mkutano wa siku mbili wa mawasilisho ya mada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maafali ya kwanza ya Chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25, mwaka huu.

katika hatua nyinge Prof. Luoga amezungumzia umuhimu wa wataalamu wa Sekta ya fedha kuendelea kufanya utafiti ili kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta hiyo ambapo amezungumzia umuhimu wa uwepo wa Chuo cha Benki Kuu kilichojikita katika kuhakikisha kinazalisha wataalamu watakaokwenda Kusimamia Sekta ya Benki.

Chuo chetu kimejikita katika kuhakikisha Sekta ya mabenki inapata wataalamu ambao watasimamia Sekta hiyo”

“Chuo chetu Kwa kushirikiana na vyuo vingine nchini vinaweza kuelekeza nguvu na juhudi za kufanya utafiti katika eneo zima la usimamizi wa Sekta ya fedha nchini”  

Hii ni Sekta ambayo inasimamiwa na Benki Kuu na ndiye mshauri Mkuu wa Serikali, ndio maana katika eneo zima la usimamizi wa Sekta ya fedha Benki Kuu lazima iwe huru kwa kushirikiana na wataalamu ambao inawategemea  kuhakikisha kuwa utafiti unafanyika na ufumbuzi unapatikana kabla athari hazijatokeza. Ndicho kitu tunachokifanya leo kuangalia tumefikia wapi katika kutayarisha wataalamu, tumefikia wapi katika kufanya utafiti, kwa kushirikiaha na wataalamu kutoka katika Taasisi nyingine kuhakikisha kuwa tunakuwa na uwezo katika kufanya utafiti kupata ufumbuzi na kutekeleza” amesema Prof. Luoga.

Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania kitafanya Maafali yake ya kwanza Ijumaa Novemba 25, 2022 toka kuanzishwa kwake na kuwa na jumla ya wahitimu 36 waliofanya vizuri na kufaulu masomo yao.