Benki ya NMB yasaidia Wahanga wa mafuriko Hanang

Benki ya NMB yasaidia Wahanga wa mafuriko Hanang

General / 7th December, 2023

Wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, Mkoani Manyara, waliopoteza ndugu zao, makazi, pamoja na mali, wamepatiwa misaada ya kibinadamu na Benki ya NMB.

Misaada hiyo inajumuisha magodoro, vyakula na vifaa vingine, ikiwa lengo ni kutoa msaada muhimu baada ya janga hilo.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus, akikabidhi misaada hiyo, amesema benki hiyo inaungana na familia za wahanga na kutoa misaada ya kibinadamu. Msaada huo unalenga kutoa faraja na msaada wa msingi ili kusaidia katika kurejesha hali ya kawaida kwa wahanga wa mafuriko.

Mbunge wa Viti Maalumu, Asia Halamga, ameipongeza benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii, hasa kwa wahanga wa mafuriko katika kipindi hiki.

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus (aliyevaa fulana nyeupe), akikabidhi misaada kwa waathirika wa mafuriko Hanang. Anamkabidhi Mbunge wa Vijana wa Hanang, Asia Halamga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.