ATCL yaongeza idadi ya safari kwenda india na china
Ili kupanua Wigo wa biashara nchini Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake za nje ya Nchi pamoja na kupunguza gharama za Usafiri wa ndege lengo likiwa ni kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa urahisi .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege (ATCL) Ladislaus Matindi wakati akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema Shirika limeamua kupanua mtandao wa safari kwa ndege zenye masafa ya mbali (Dream liner) zinazofanya safari kutoka Tanzania kwenda India na nyingine kutoka Tanzania kwenda China.
Aidha Matindi amesema Kuongezeka kwa safari hizo pamoja na kupungua kwa gaharama kwenda nje ni kutokana kupunguzwa kwa masharti ya UVICO_19 hivyo sasa safari za kwenda China zitakuwa mara mbili kwa wiki na kwenda India itakuwa mara nne kwa wiki.
Mbali na hayo Matindi amesema ili kuendelea kuboresha Shirika Hilo hivi karibuni Ndege mbili zinatarajiwa kufika nchini mwaka huu ambapo Ndege moja itaingia mwezi wa nane na mwisho wa mwaka huu
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za Ajira zilizopo kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kama vile uhasibu, uhudumu wa kwenye ndege, Urubani na nyingine nyingi ambazo zitatokea kupitia ujio wa ndege hizo mpya.
Ikumbukwe kuwa shirika la ndege Tanzania lilipunguza safari zake za nchi ya nje baada ya kuwepo kwa janga la ugonjwa wa COVID-19 lililoingia nchini 2020.