Waziri Stergomena ataka Mafunzo ya manunuzi yawajengee weledi washiriki

Waziri Stergomena ataka Mafunzo ya manunuzi yawajengee weledi washiriki

General / 10th August, 2022

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amewataka washiriki wa Mafunzo yanayohusu Manunuzi ya Umma kuhakikisha kuwa Mafunzo hayo yanawajengea Weledi na kuwawezesha kutekeleza Shughuli za manunuzi ya Umma kwa Uaminifu na Uadilifu.

Mheshimiwa Waziri ameyasema hayo katika Ukumbi wa JKT Chamwino alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku mbili yanayohusisha Afisa Masuuli, Idara na Virengo tumizi, bodi za zabuni na Kamati ya ukaguzi ambapo pamoja na mambo mengine mheshimiwa Waziri kasisitiza kuwa Mafunzo haya ni muhimu sana iwapo mhusika hayupo tutakuwa tunapoteza fursa muhimu saana.

Waziri amesema Sekta ya manunuzi ni sekta muhimu sana katika Wizara na Taasisi mbalimbali, ufanisi katika manunuzi ya umma ni mhimiri katika ufanisi wa taasisi kwani kila mwaka Serikali hutenga fedha nyingi kwa ajili ya manunuzi, wakati wote ni matumaini ya Serikali kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa na manunuzi yaliyozingatia taratibu, ubora na thamani ya fedha.

Waziri pia amewakumbusha washiriki wa mafunzo haya kuyatumia vizuri kwa kutanguliza maslahi mapana kwa nchi pindi wanapotekeleza majukumu yao ya msingi.

Aidha, Mheshimiwa Waziri amesema Mafunzo haya yanayotolewa na Wawezeshaji kutoka Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi ya Umma – PPRA yana lengo la kuwajengea uwezo taasisi za manunuzi ya Umma ambazo kwa mijubu wa sharia ya mwaka 2011 ikafanyiwa marekebisho mwaka 2016 na kurekebishwa tena mwaka 2022 zimepewa mamlaka tangu kuandaa bajeti na kuanzisha mahitajio hadi kukamilisha kwa manunuzi.