TBS yawataka wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kwa mazoea.

TBS yawataka wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kwa mazoea.

Business / 17th May, 2022

Wafanyabiashara nchini wametakiwa kulenga masoko ya biashara zao kimataifa kwa kuzingatia uwekaji wa nembo ya TBS  Katik bidhaa zao na kuachana na tabia ya kufanya biashara kimazoea

Wito huo umetolewa  Mkoani Morogoro na Afisa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango nchini(TBS) Bwana Hassani Juma kwenye maonesho ya tano ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Akizungumza na Michuzi Blog Bwana Hassani aliwataka wafanyabishara kuacha tabia ya kupeleka bidhaa sokoni bila ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kwani kufanya hivyo ni kosa kishria na adhabu yake ni bidhaa zao kutekezwa na utozwaji wa faini.

Adha amesema mbali na kuwa ni kosa kisheria lakini pia kukosa kuweka alama ya udhibiti ubora kunazikosesha bidhaa zao uhalali sokoni.

Kwa upande wao wakazi wa Mkoa wa Morogoro waliotembelea banda la shirika hilo katika viwanja vya Jamhuri wamelipongeza shirika kwa elimu wanayoitoa kwa wananchi   juu ya Umuhimu wa kusajili Bishara na kupata alama ya uthibitisho wa ubora katika bidhaa zao kwani kunaongeza thamani ya bidhaa.

Waliieleza Michuzi Blog wakazi hao wamesema licha ya kusogezewa huduma kwa ukaribu zaidi hivi sasa wanatambua umuhimu wa kuwa na alama ya TBS kwani itawasaidia kuondosha usumbufu wakati wa uuzaji wa bidhaa zao.

Aidha wamesema kupitia elimu inayotolewa na TBS inawaongezea ueledi wa utanuzi shughuli zao za biashara ndani na nje ya nchi kwani wamekuwa wakitambuliwa kimataifa kupitia majina ya bidhaa na kampuni zao.