Sheria zinacholewesha mashauri ya kiuchumi kufanyiwa marekebisho

Sheria zinacholewesha mashauri ya kiuchumi kufanyiwa marekebisho

General / 1st February, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kufanyia marekebisho sheria  zote zenye mizunguko zinazochelewesha kesi na upatikanaji wa haki kwa mapema  kwani kucheleweshwa kwa kesi hupelekea kucheleweshwa kwa haki


Amesema hayo leo Februari 2,2023 Jijini Dodoma, wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini yenye kauli mbiu "Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi  endelevu, wajibu wa maharaja na wadau"


"Mashauri mengi hasa yanayohusu uchumi kama fedha na kodi, yanapitia hatua nyingi sana mpaka kukamilika kwake, kwahiyo Wizara husika, wadau pamoja na Jaji Mkuu fanyieni marekebisho hizo sheria zote zenye mizunguko mingi" amesema Samia


Aidha, amesema kuwa Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa nchi kupitia fursa za uwekezaji na biashara ambazo zinaushindani nchini, ambapo kumekuwa na migogoro mingi inayohitaji usuluhishi


"Tumefungua Tanzania kuwa kitovu cha biashara ndani ya nchi na ukanda wa Afrika Mashariki lakini hata kusini mwa Afrika na tumekuwa tukivutia wawekezaji kila tunapokwenda nje ya nchi yetu na kwa bahati nzuri, tumekuwa tukiitikiwa vyema na sasa wote wanapokuja wanataka kuona haki inatendeka katika biashara zao, wanapowekeza fedha zao na kufanya mawasiliano na taasisi mbalimbali za nchi yetu" amesema Samia


Ameongeza kwa kusema kuwa kuna umuhimu wa kuimarisha mifumo ya utoaji wa haki, ili kutatua migogoro kwa haraka na hatimae kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara kwa kujenga imani ya usalama wa mali zao.


Rais Samia amemtaka Jaji mkuu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, kutokana na umuhimu mkubwa wa suala hilo katika kipindi hiki cha nadharia ya usawa wa kijinsia, uchumi na ushindani pia kupunguza gharama za kifedha na muda mwingi unaotumika katika ufuatiliaji wa kesi.


Itakumbukwa kuwa maadhimisho hayo kwa mujibu wa kaulimbiu, yanalengo la kupunguza msongamano wa mashauri mahakamani na pia kuweka amani baina ya wa daawa.