Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Freeman Mbowe

General / 4th March, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe.

Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi a haki. Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kuiali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taifa la Tanzania ni kusimama katika haki

Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na za kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipaswavyo.