Rais Samia afanya mabadiliko ya Mawaziri

Rais Samia afanya mabadiliko ya Mawaziri

General / 1st April, 2022

Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri ambayo yamehusisha uhamisho wa mawaziri watatu.

 

Katika mabadiliko hayo aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria , George Simbachawene amehamishwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu huku nafasi yake ikichukuliwa na Damas Ndumbaro.

 

Waziri Ndumbaro yeye amehamishwa kutoka kuwa Waziri wa Mali asili na utalii nafasi ambayo sasa imechukuliwa Pindi Chana ambaye kabla ya hapo alikuwa Waziri wa Bunge, Sera na Uratibu.

 

Katika taarifa iliyotolewa leo Machi 31, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa mabadiliko hayo yaanza mara moja