Nyati aua watu watatu Mtwara

Nyati aua watu watatu Mtwara

General / 24th March, 2022

Watu watatu kutoka vijiji tofauti mkoani Mtwara wameuawa kwa kuchomwa na nyati ambaye ameingia katika makazi ya watu.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo leo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Machi 20.


Katembo aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Rashid Bakari 40 mkazi wa Kijiji cha Kitunguli, Salum Yusuf 46 na Said Musa 45 wakazi wa Kijiji cha Mahurunga.


Alisema walivamiwa na nyati ambaye alifika ghafla kijijini hapo akitokea vichakani.
Nyati huyo aliyezurura aliuawa baadaye na polisi. Baada ya uchunguzi kukamilika miili ya marehemu ilikabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi.