NMB Yaahidi Kuendeleza Kunufaisha Sekta Ya Kilimo Nchini

NMB Yaahidi Kuendeleza Kunufaisha Sekta Ya Kilimo Nchini

General / 11th August, 2022

Benki ya NMB imeweka adhma ya kuendelea kuiboresha sekta ya kilimo nchini kwa kutoa masuluhisho bora na nafuu kwa shughuli za kilimo na zilizo katika mnyororo huo wa thamani.

Benki hiyo imetoa zaidi ya Bilioni 509 mwaka huu na wametenga zaidi ya Bilioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa maghala kuondoa upotevu wa mazao ya wakulima ambazo mpaka sasa jumla ya Bilioni 6 zimetolewa kwa wakulima kwenye vyama vya ushirika (AMCOS).

Aidha, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB- Bw. Filbert Mponzi alisema, kwa kipindi chote cha Nane Nane wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima mbalimbali kwenye banda lao bure ili kuhakikisha wanapata mafunzo yatakayo wawezesha kutunza fedha,kukuza mitaji ya kilimo,ufugaji na uvuvi na kupata fursa za mikopo.

Lakini pia, benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora zenye ufanisi na zinazoendana na matakwa ya wateja wake huku wakiendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha malengo ya kiuchumi ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.

Benki ya NMB imeshiriki maonesho ya nanenane ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kilele chake cha siku ya nanenane.

 


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biasharawa NMB- Bw. Filbert Mponzi(katikati) akizungumza kwenye maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika jijini Mbeya. Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa NMB- Bw. Isaac Masusu(kushoto) pamoja na Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu wa NMB- Straton Chilongola.