NIC Yatoa Gawio Kwa Serikali

NIC Yatoa Gawio Kwa Serikali

Business / 21st April, 2022

Shirika la Bima la Taifa NIC limetoa  gawio  ya Sh.Bilioni 1.5 kwa Serikali baada ya kufanya vyema kwa miaka minne mfululizo na kuweza kupata faida ambayo imekwenda kutoa gawio hilo.

Shirika hilo kutokana na faida hiyo inakwenda kuongeza   mitaji na shirika wa Bilioni 12.05 ambapo kunafanya NIC iweze kuwa na uwezo mkubwa ushindani katika soko .
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 20,2022 Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NIC,  Laston Msongole amesema kwa kipindi cha miaka minne mfululizo iliyopita kwa hesabu zilizokaguliwa inayonyesha kufanya vizuri baada ya taarifa ya hesabu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za  Serikali (CAG).

Amesema shirika  limeendelea kuwa imara kwa  kuongeza faida ambapo shirika hilo halijawahi kutoa gawio kwa serikali kwa miaka 30 iliyopita.

“Miaka minne mfululizo iliyopita kufikia mpaka Juni, 2021 ambapo tunahesabu zilizokaguliwa, Shirika limekuwa na maendeleo yakutosha na hilo linathibitishwa na taarifa CAG  ampapo kila mwaka anakagua”. Amesema

Amesema katika kipindi cha mwaka 2018, Shirika lilipata faida ya bilioni 3.63, mwaka uliofuatia ambao ni 2019 likapata bilioni 7.79, mwaka 2020 likapata bilioni 33.65 na mwaka unaoishia Juni,2022 wamepata bilioni 73.10 hivyo Shirika  limeendelea kuongeza faida kila kukicha.

Aidha Msongole amesema kuwa matarajio yao kufikia mwakani kwa maana hesabu za kukaguliwa kufikia Juni 2022 hesabu hiyo itakuwa mbali na hiyo ambayo wamefikia kwa sasa.

Pamoja na hayo amesema kwa mafanikio hayo waliyoyapata wanatarajia kutoa gawio kwa Serikali kutokana na mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kwa miaka minne kwa kuongeza mtaji.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina Mgonya Benedicto amesema Shirika hilo limejiweka vizuri katika kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kwa wakati huohuo limeendelea kujenga imani kwa watanzania ambapo hivi sasa ni idadi kubwa kwa wanaokata bima kwenye shirika hilo.

Ameeleza kuwa katika majadiliano yao kupitia mahesabu ya shirika, ile faida ambayo imepatikana sehemu wameamua kuimarisha mtaji wa shirika ambapo sasa utaiwezesha kufanya bioiashara kisheria ukilinganisha na hapo awali vilevile wamekubaliana shemu nyingine ipelekwe kwenye mfuko wa serikali kama gawio kwa serikali.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk. Elirehema Doriye amesema moja wapo ya mipango ambayo wamekuwa nayo kwa sasa ni katika uharaka wa utoaji huduma za Bima, kwasasa NIC linatoa huduma za Bima kwa maana ya ulipaji wa madai kwa muda mfupi kuliko shirika au kampuni yoyote Tanzania, ndani ya siku tano za kazi unapata malipo yako.

Amesema fedha hiyo inakwenda kwenda kuimarisha huduma ili kwenda kwa kasi zaidi na watu wataopata huduma kuwa sehemu ya mabalozi kutokana na ubora wa huduma zilizo NIC.

Amesema kwa mafanikio hayo yanatokana na  wafanyakazi kufanya kazi kwa kujitoa vipawa vyao ikiwemo ubunifu.

Msajili wa Hazina Mgonya Benedicto (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika Shirika la Taifa la Bima (NIC) kuhusiana na maendeleo ya Shirika hilo pamoja na kutoa gawio kwa Serikali jijini Dar es Salaam kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa NIC Laston Msongole watatu kutoka kushoto ni Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Laston Msongole akizungumza kuhusiana na mafanikio ya Shirika hilo kwa miaka minne mfululizo jijini Dar es Salaam.katikati ni Msajili wa Hazina Mgonya Benedicto na watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dk.Elirema Doriye.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza mafanikio ya Shirika hilo kuhusiana na kutoa gawio kwa Serikali pamoja na kujiimarisha katika kutoa huduma bora za bima nchini,jijini Dar es Salaam.