Hatua zilizochukuliwa kukabiliana na mfumuko wa Bei

Hatua  zilizochukuliwa kukabiliana na mfumuko wa Bei

General / 1st February, 2023


Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali haijajificha kwenye vita ya Ukraine na Urusi, uviko na mabadiliko ya tabianchi katika suala la mfumuko wa bei nchini kwa kuwa mambo hayo ni halisia na Serikali imeendelea kuchukua hatua.

Dkt. Nchemba amebainisha hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa kwa Mbunge wa Arusha Mjini  Mrisho Gambo, aliyesema kuwa Serikali inajificha katika vita ya Ukraine na Urusi katika suala la mfumuko wa bei.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imechukua hatua ambazo nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika hazijazifikia

“Kwa ujumla hamna nchi imechukua hatua ya kutoa bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kupunguza gharama, ndio maana hata nchi jirani zinakimbilia Tanzania kuchukua vitu”, alisema Dkt. Nchemba.

Alisema kuwa Serikali imeondoa tozo na kodi zote katika mafuta ya kula na ikachukua nusu ya gharama ya bei ya kila mfuko wa mbolea na bado Serikali ina jitihada nyingineinazoendelea kuchukua na inaendelea kuwa makini katika jambo hilo.