Hati Fungani ya 'NMB Jasiri' yaorodheshwa rasmi katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE).

Business / 28th April, 2022

Serikali imesema kitendo cha benki ya NMB kuvunja rekodi katika uuzaji wa hati fungani za JASIRI kwa asilimia mia tatu kutoka kwenye malengo waliojiwekea ya billion 24 hadi kufikia billion 74.3 inadhihirisha wazi kuwa uelewa wa watanzania juu ya hati fungani unazidi kukuwa.

 

Aidha billion 74.3 zilizopatikana baada ya NMB kuuza hati fungani kwa kipindi cha wiki sita, asilimia 99 ya hati fungani hizo zimenunuliwa na wawekezaji wa ndani ya nchini kati ya hao asilimia 52 wakiwa ni wanawake, asilimia 83 ya uwekezaji huo umefanywa na watanzani walio nje ya dar es salaam, na asilimia 96 ya wawekezaji wamenunua hati fungani zao kwenye matawi ya benki ya NMB yaliyosambaa kote nchini.

 

Akionga muda mfupi baada ya kugonga kengere ya kuashiria uorodheshaji rasmi kwenye soko la hisa la dar es salaam na ufungaji rasmi wa ununuzi wa hati fungani za JASIRI, naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango Lawrence Mafuru, amesema kitendo cha asilimi 83 ya wawekezaji wa hati fungani za jasiri kutoka nje ya dar es salaam, ni ishara wazi kuwa mzunguko wa fedha umesambaa kote nchini, tofuati na ilivyokuwa hapo awali ambapo wanunuzi wakubwa wa hati fungani hizo walikuwa wanatoka jijini dar es salaam.

 

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana nchini Nicodemus Mkama, amesema hati fungani hii ya JASIRI ni chachu kubwa ya maendeleo ya sekta ya fedha hapa nchini, huku akibainisha kuwa kuwa asilimia 99.9 ya wawekezaji kwenye Hati fungani ya Jasiri ni wawekezaji wadogo wadogo.

 

Nae Afisa mtendaji mkuu wa benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema uuzaji wa hati fungani hizo ulilenga kukusanya billion 25, lakini kutokana na Imani kubwa waliyonayo watanzania kwa benki ya NMB wameweza kukusanya jumla y ash billion 74.3, ambazo zinakwenda moja kwa moja kunufaisha wanawake wa Tanzania kiuchumi.

 

Fedha Billion 74.3 zilizopatikana baada ya uuzaji wa HISA ZA JASIRI uliofanywa na benki ya NMB kwa kipindi cha miezi sita, zinakwenda moja kwa moja kutoa mikopo ambayo itaboresha biashara zinazoendeshwa na wanawake au shughuli yoyote ile ambayo wanufaika wakubwa ni wanawake.