Hafla ya Utiaji saini wa Makubaliano kati ya Equity Group Foundation, Equity Bank Tanzania na MIF (MWANAMKE INITIATIVE FOUNDATION)

Hafla ya Utiaji saini wa Makubaliano kati ya Equity Group Foundation, Equity Bank Tanzania na MIF (MWANAMKE INITIATIVE FOUNDATION)

General / 21st November, 2022




Leo tarehe 21/11/2022 inafanyika hafla ya Utiaji saini wa Makubaliano kati ya Equity Group Foundation, Equity Bank Tanzania na MIF (MWANAMKE INITIATIVE FOUNDATION) iliyoanzishwa na Mh Wanu Hafidh Ameir ambae pia ni mbunge wa bunge la jamuhuri la muungano la Tanzania katika Hoteli ya Serena, Dar Es Salaam ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Dk. James Mwangi, CEO wa EQUITY GROUP.

 

MIF ni shirika lisilo la serikali na lisilo la faida lililoanzishwa kwa lengo la kuweka mfumo wa kuunda mazungumzo yanayoweza kutekelezeka, mitandao, habari na kubadilishana ujuzi kuhusu ustawi wa wanawake, vijana na watoto katika afya, elimu na nyanja za kiuchumi za kijamii.

Ubia huo unalenga kuisaidia MIF katika Elimu ya Kifedha na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa makundi yanayolengwa kutoka sekta mbalimbali kama vile Kilimo, Afya, Elimu n.k.

 

Kwenye sekta ya kilimo,

Tutahakikisha wakulima wanakuwa katika mfumo rasmi wa kilimo ili waweze kuhudumiwa mahitaji yao na kuwaongezea mnyororo wa thamani wa bidhaa zao.

 

Kwenye sekta ya Afya,

Tutahakikisha tunaongeza weledi kwa watoa huduma wa afya ili mama na mtoto wapate huduma sahihi tukianza na afya ya uzazi.

 

kupitia mkataba huu Equity benki watasaidia kuimarisha Ufuatiliaji, tathmini,mafunzo,utoaji taarifa ili kuhakikisha utendaji wa MIF na miradi yake inakuwa katika kiwango cha juu cha utekelezaji.

 

Pia Equity benki itatusaidia Ujengaji wa uwezo kwa wafanyakazi wa MIF juu ya maswala ya fedha na uandaaji wa ripoti.Itatoa msaada na ushirikiano katika Nyanja za wafanyakazi wenye sifa watakaofanya kazi moja kwa moja na MIF katika maeneo mbali mbali kama

• Fedha na udhibiti

• Uandaaji wa rasilimali fedha

• Ufuatiliaji na tathmini ya miradi na programu za Taasisi

 



 

Imetolewa na;

Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Equity Bank.