CRDB kusimamia Mfuko wa Faida Fund

CRDB kusimamia Mfuko wa Faida Fund

General / 15th January, 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amezitaka Taasisi zinazohusika na Maendeleo ya vijana, wanawake na makundi maalum kuanza kuyahamasisha makundi hayo kuwekeza kwenye Mfuko wa Faida uliopo chini ya Shirika la Watumishi (Watukishi Housing Investiments), ili asiwepo mtanzania wakuachwa nyuma katika shughuli za uwekezaji na ukuzaji wa mitaji.


Mhe. Mhagama amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Mfuko huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam, na kusema kuwa mfuko huo ni salama kwa uwekezaji kwani tangu uanzishwe hadi sasa umeonesha mafanikio makubwa kwenye sekta ya uwekezaji na uchumi.

Aidha amebainisha kuwa umiliki wa mfuko huo haubagui kufuatia kiwango cha chini cha uwekezaji kuwa ni kuanzia elf 10 hivyo unatoa fursa Kwa mtanzania yoyote kujiunga.


Kwa upande wa Mtunza Amana wa Mfuko wa Faida (Faida Fund) ambaye ni Benki ya CRDB kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Abdulmajid Nsekela ameeleza kwamba mfuko huo ni wa kipekee, kwani umezingatia sera mahususi ya huduma jumuishi za kifedha zinazomjali mtanzania wa rika zote ikiwa ni pamoja na kuweza kununua vipande kwa shilingi elfu 10 jambo ambalo linaenda sambaba na sera ya benki hiyo ya kumsikiliza mteja.

Amebainisha kuwa Benki ya CRDB inachangia Zaidi ya asilimia 70 ya wateja wote wanaoshiriki katika masoko ya mitaji na dhamana ambapo Soko la Hisa la Dar es Salaam-DSE  kupitia tuzo zake inaitabmbua benki hiyo kama kinara wa huduma bora kwenye masoko ya mitaji.

 
Katika hatua nyingine amefafanua kwamba, Mfuko wa Faida unakuwa mfuko wa saba katika mifuko ya uwezazaji wa pamoja ambayo benki ya crdb inaisimamia na unatoa fursa pekee ya uwekezaji wa muda mfupi kwa watanzania kuweza kukuza mitaji yao kwa faida lakini pia ni faida kwa watumishi housing kukusanya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.